Dodoma/Dar es Salaam. Wabunge 160 wa CCM
wamejiorodhesha kuomba kuitishwa kwa kikao cha Kamati ya Wabunge hao kwa
lengo la kuwajadili mawaziri wanaotajwa kuwa mizigo.
Pia wabunge hao wanataka Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahaman Kinana naye awepo kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Kamati ya Wabunge
wa CCM, Hussein Mussa Mzee, alimwambia mwandishi wetu kuwa wamepokea
barua iliyoambatana na orodha ya majina ya wabunge zaidi ya 160 waliotia
saini kutaka kuitishwa kwa kikao hicho.
“Hata kama wangesaini wabunge 10 tu tungeitisha
kikao. Bahati nzuri walisaini zaidi ya 160, kwa hiyo kikao kitaitishwa
kwa kuwa ni haki yao kikanuni kutaka kukutana,” alisema.
Alipoulizwa kwa nini kikao hicho hakikuitishwa
ndani ya wiki moja ambao ndiyo muda wabunge hao walioutaka kabla ya
Kamati Kuu ya CCM kukutana wikiendi iliyopita, Mzee alisema hiyo
lilitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, kutokuwapo bungeni.
Mzee alisema pia kikao hicho kilishindwa kufanyika
mara ya kwanza kutokana na Kinana kuwa safarini Afrika Kusini ambako
alihudhuria mazishi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Hata hivyo, alisema hawezi kujua ni lini kikao
hicho kitafanyika lakini aliahidi kuwa itakuwa mara baada ya Kinana
kurejea nchini.
Wiki iliyopita, gazeti hili liliandika kuhusu wabunge wa CCM kujiorodhesha ili kushinikiza kufanyika kwa kikao hicho.
Chanzo kimoja cha kuaminika kilisema kuwa fomu
hiyo iliwasilishwa katika Ofisi ya Katibu wa Wabunge wa CCM ikiambatana
na barua inayotaka kuitishwa kwa kikao kitakachowakutanisha.
“Tuliwaomba waitishe kikao cha wabunge wa CCM ili
mawaziri ambao tunawaona hawatimizi majukumu yao kikamilifu waweze
kuhojiwa lakini wakawa wanasuasua,” kilisema chanzo hicho.
Kikao hicho kilitakiwa kufanyika Alhamisi iliyopita ili kuwahoji mawaziri hao kabla ya kikao cha Kamati Kuu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
alikaririwa wikiendi hii akieleza kuwa mawaziri saba walihojiwa katika
kikao cha Kamati Kuu na kumuachia Rais Jakaya Kikwete jukumu la kuamua
kuwafukuza kazi, kuwahamisha au kuwataka kutekeleza majukumu yao
kikamilifu.
Chanzo cha habari: Gazeti la Mwananchi.
Chanzo cha habari: Gazeti la Mwananchi.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation.
0 comments:
Post a Comment