Kiwango cha sasa cha ukuaji wa uchumi ni asilimia 7, kiwango cha kupungua umasikini ni asilimia 2, jambo ambalo linaonesha kuwa kila juhudi inachukua mwelekeo wake.
Rais Kikwete alisema kutokana na asilimia 75 ya Watanzania, kuachwa mbali na faida za ukuaji wa uchumi, unaochangia kuongezeka kwa tofauti ya usawa.
“Changamoto kubwa ni kilimo... sekta zingine zinaongezeka kwa karibu asilimia 20, lakini si kilimo ambacho kinakua kwa asilimia 4.3,” Rais alisema jana wakati wa kufungua Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara.
Alisema kushindwa kuinua kilimo, uvuvi na ufugaji, kunaendelea kushusha juhudi za ukuaji wa Pato la Taifa kwa zaidi ya asilimia 10.
“Kama tutafanikiwa kujumuisha sekta ya kilimo katika uchumi kwa angalau asilimia sita, ukuaji wa Pato la Taifa utakuwa kwa kasi mpaka asilimia 10 na zaidi … na utaweza kuona matokeo yake,” alisema Rais ambaye ni Mwenyekiti wa TNBC.
Rais Kikwete alitaja baadhi ya ufumbuzi wa matatizo ya kilimo, ikiwa ni pamoja na serikali kufanya wajibu wake katika sera na kutambua vikwazo inavyokabili sekta hiyo, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi na kushiriki ipasavyo kwa sekta binafsi.
“Sekta binafsi inapaswa kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo wakati kusambaza pembejeo na vifaa vingine kusiwanyonye wakulima,” alisema Rais, ambaye alihudhuria mkutano huo akitokea moja kwa moja Afrika Kusini, alikokwenda kwa ajili ya maziko ya Nelson Mandela.
Alisema majadiliano katika mkutano huo, yanatakiwa kulenga katika ustawi wa taifa na si ubinafsi.
Chanzo cha habari: Gazeti la HabariLeo
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation.
0 comments:
Post a Comment