Mwaka 2011,nilipata kufuatilia kwa
ukaribu kuhusu mitandao ya kijamii.Nilipata muda wa kuchambua mtandao mmoja
baada ya mwingine,nilipaswa kufanya hivyo ili kubaini ni nani ni gwiji kati ya mitandao
hiyo.Nilipata kujua tofauti kati ya mtandao mmoja na mwingine,na kwanini mtu
utumie mtandao huu na usitumie mwingine.Na mwisho wa siku nilikuja kutambua ya
kwamba Facebook ndiyo ulikuwa mtandao uliotengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu,na
unaotoa huduma nyingi zaidi ukifana nisha na mitadano mingine,kama twitter,
linked in ,my space na mitandao mingineyo.Uchunguzi huo ulinichukua
muda,takribani mwezi mmoja.
Matumizi ya mitandao ya kijamii
imebadili maisha ya watu wengi sana,haswa namna ya upashanaji habari.Taarifa
zimekuwa zikiwafikia watu wengi sana ndani ya muda mfupi,na vyanzo vya habari
vimeongezeka,ukilinganisha na miaka ya nyuma,na hii ni changamoto kwa TCRA
katika kudhibiti ubora na ukweli wa habari zinazowafikia mamia ya watu.
Kuongezeka kwa watumiaji wa mitandao
ya kijamii,ni ishara tosha ya kwamba watanzania walio na uelewa juu ya matumizi
ya internet unaongezeka,ni jambo jema hilo,ingawa tunapaswa kujiuliza maswali
ya msingi,je watumiaji wa internet wanatumia kwa usahihi,na je tunatumia viwango(standards) vipi kuamua ya kwamba mtu
huyu anatumia kwa usahihi na huyu hatumii kwa usahihi.Hayo yote tunapaswa
kutafakari na kuchukua hatua.
Watumiaji wengi wa mitandao ya
kijamii ni vijana na wengi wao hutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuchart,kupost
picha ambazo hazina mantiki na nyingi ni picha ambazo zimekosa maadali. kitu
ambacho kinawapotezea muda mwingi,na kuharibu fikra zao na kupunguza uwezo wao
wa kujikita katika masuala ya msingi,matokeo yake tumekuwa na vijana wengi
ambao hawajikita katika kujiletea maendeleo yao binafsi. Kuna fursa nyingi sana
kwenye mitandao ya kijamii,iwapo tu mtumiaji ataamua kutumia mitandao ya
kijamii kama sehemu ya kujitengenezea fursa.
Na ni wito wangu kwa vijana kutumia
mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujitengenezea fursa za maendeleo
yao.Tusipoteze muda kwenye masuala ambayo si ya msingi pindi tunapokuwa
internert bali tutumie muda wetu kwenye kujifunza na kudadisi masuala ya msingi
yanayoweza kutufanya tuanze kujiletea maendeleo.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation.
0 comments:
Post a Comment