Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Vermaas alisema kadi hiyo itamwezesha mfanyakazi kupata mshahara wake moja kwa moja pindi unapoingizwa benki na taarifa atazipata kupitia simu yake ya mkononi.
Alisema lengo la kadi hiyo ni kumwezesha mfanyakazi kutopata usumbufu wa kwenda kupanga foleni kuchukua mshahara wake benki.
Aidha alisema kwa sasa wana mkakati wa kuhakikisha kila sehemu yenye wafanyakazi wengi, mwajiri akikubali mpango huo wataweka mashine za kutolea huduma ya B-Pesa.
Alisema kadi ya B-Pesa inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo uhamisho wa fedha kwenye kadi, kutolea fedha, kuingiza fedha na kulipia bili, kununua bidhaa na kulipa huduma mbalimbali.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation.
Hii itakuwa nafuu kwa wafanyakazi.
ReplyDelete