Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, limekiri
kutikiswa na ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imemkumba
Waziri wake wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya
Mungulu alisema jana kwamba operesheni hiyo imelitikisa jeshi hilo
kutokana na madhara yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wake.
“Lengo la operesheni hiyo halikuwa kuleta madhara
kwa wananchi, yaliyotokea ni changamoto kwa Polisi na sasa ni kujipanga
upya ili haya yasije kutokea tena,” alisema na aliongeza: “Kwa sasa
tunaziachia mamlaka husika ziendelee kulishughulikia suala hili kwa
sababu limehusisha idara mbalimbali za Serikali.”
Kauli hiyo, imekuja baada ya ripoti iliyosomwa
bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira, James Lembeli ambayo imesababisha Rais Jakaya Kikwete
kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Kauli hiyo, imekuja baada ya ripoti iliyosomwa
bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira, James Lembeli ambayo imesababisha Rais Jakaya Kikwete
kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Mapema Novemba, mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne
Makinda aliunda Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
kuchunguza utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili baada ya kutokea
mjadala mkali bungeni kuhusu kadhia waliyopata wananchi.
Katika mjadala huo, wabunge walilalamikia
watekelezaji wake wakisema ilitawaliwa na mateso kwani waliokuwa
wakiiendesha walikuwa wakiwatesa wananchi na hata kusababisha vifo na
majeruhi.
Taasisi zilizokuwa zikiendesha operesheni hiyo kabla ya kusitishwa ni; Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi.
Kuzinduliwa kwa operesheni hiyo kulikuwa na lengo
la kulinda rasilimali za nchi hasa tembo ambao katika siku za hivi
karibuni wamekuwa wakiuawa kwa kasi na majangili kwa ajili ya pembe za
ndovu.
Credits: Mwananchi Gazeti
Credits: Mwananchi Gazeti
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation.
0 comments:
Post a Comment