Tunaishi
katika dunia ambayo mabadiliko ya kiuchumi na teknolojia ya naongezeka kwa kasi
kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.Mifumo yote miwili (Uchumi na
teknolojia) ndiyo inayopelekea watu wa jamii fulani wawe na mfumo wa aina fulani
wa maisha. Kwa mfano jamii iliyo na uchumi imara,utoa uhakika wa upatikanaji wa
ajira na huduma muhimu katika jamii kama
vile upatikanaji wa elimu,huduma za afya,miundo mbinu imara.
jamii yenye uchumi
imara ni jamii yenye watu wenye afya njema,na maisha bora,na fikra zao huwa ni
fikra zisizo na mawaa ya ajabu ajabu,na mara nyingi jamii zenye uchumi imara
zina teknolojia ya hali ya juu,ukifananisha na jamii zenye uchumi ambao si
imara.Mataifa ambayo uchumi wake umedorora hukumbwa Zaidi na matatizo ya
ajira,Vijana wanapaswa kuelewa kwamba kinachotoa ajira si mfumo wa kisiasa,bali
ni mfumo wa uchumi,mfumo ukiwa m’bovu basi ajira itakuwa ni tatizo, bali uchumi
ukiwa imara tatizo la ajira litakuwepo kwa kiasi kidogo.
Maendeleo ya teknolojia
ya mawasiliano “Information Technology”
katika miaka ya hivi karibuni yamekuwa kwa kasi kubwa sana,na ata kubadili
mfumo wa maisha ya kijamii baina ya mtu na mtu,mathalani mitandao ya
kijamii(kama facebook,twitter,blogs)imepelekea kubadili mfumo wa upashanaji wa
habari katika jamii.Leo hii mtu yeyote aliye na ufahamu wa kutumia
internet,anaweza akawa chanzo cha habari(Source
of information),na habari atakayo itoa ikawafikia maelfu ya watu ndani ya
dakika chache sana.
Si tu kwamba teknolojia
ya mawasiliano imebadilisha mfumo wa upashanaji wa habari,bali pia ata shughuli
za kiuchumi.Siku za hivi karibuni tumekuwa mashahidi na kujionea mifumo ya
mawasiliano “Information systems”
ikifungwa katika taasisi mbalimbali “organizations”,leo si kitu cha ajabu, kwa
benki kuwa na “information security
system”, hospitali kuwa na “hospital
management information system”,vyuo na shule kuwa na “students information system”, maduka makubwa kuwa na “store reservation system”.Hali hiyo
imepelekea mfumo mzima wa utendaji kazi wa organizations
hizo kubadilika kabisa na ata kupelekea mfumo wa uchumi wa taifa kubadilika.
Mataifa kama Marekani
yameendelea sana katika technolojia ya mawasiliano.Teknolojia ya mawasiliano
imekuwa si sehemu ya maisha bali ni maisha halisi ya kila siku,kuna baadhi ya
maeneo ukienda katika mataifa ya wenzetu ukiwa na fedha cash,unaweza usinunue
chochote kwani mfumo wa malipo umekuwa wa kidijitali sana “Pure digital payments systems”,yaani fedha zina amishwa tu kutoka
akaunti moja kwenda nyingine,kulingana na manunuzi yaliyofanyika,pasipo mnunuzi
kulipa moja kwa moja.
Tunakoelekea dunia
nzima,inalazimishwa kuingia katika mfumo wa “digital economy”.Teknolojia ya mawasiliano ndiyo itakuwa nguzo mama
wa mfumo huo wa uchumi,aliye na teknolia ya hali ya juu Zaidi ya mwenzake,ndiye
atakaye kuwa na uchumi mzuri Zaidi ya mwenzake na kuwa kinara wa
maendeleo,waswahili wana kwambia “Mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama”.Tukifia
hatua hiyo shughuli zote za uchumi zitakuwa za kidijitali na zinazoendeshwa kwa
mifumo ya kielekronia,na hivyo basi tutakuwa na mataifa yanayotegemea na
kuendeshwa na digital economy.
Mataifa makubwa,yalisha
tuacha maili nyingi tu za kutosha katika mbio hizi za teknolojia ya
mawasiliano.Taifa kama marekani lina makampuni mengi sana ya nayojihusisha
teknolojia ya mawasiliano,mfano kama google, Facebook, Microsoft, apple.
Hakuna sababu ya kukata
tamaa ata kama tumeachwa mbali sana, tunachopaswa kutambua maisha ni sasa na
wakati wa kuamka ndiyo huu,leo kila mmoja wetu anapaswa aanze kujifunza kutumia
teknolojia ya mawasiliano kwa manufaa zaidi na kwa kujitengenezea fursa za
kiuchumi,kijamii na ata kisiasa,moja ya sababu ya Obama kushinda uchaguzi wa
marekani mwaka 2008,ni jinsi alivyoendesha kampeni yake kwa njia ya kidijitali
“21st century campaign”
kitu ambacho mpinzani wake John McCain hakufanya,kuna haja ya kujifunza kutumia
internet kama chombo cha kujitengenezea
fursa.Mfano mzuri hapa Tanzania ni mjengwablog.com,situ kwamba ni sehemu ya
kupata habari bali imekuwa ni ajira kwa wale ambao wanaofanya kazi na
Maggid mjengwa.
Swala la msingi ni
jamii nzima kuhamasishwa kuwa na matumizi ya teknolojia,katika njia ambayo ni
sahihi zaidi na yenye manufaa kwa maisha yao na vizazi vyao vijavyo.Wanafunzi
wanaosoma masomo ya teknolojia,wanapaswa kuumiza bongo zao,ili waibuke na
ubunifu utakao tatua matatizo sugu katika taifa letu.
Jamii yetu ikihamasika
na kuanza kutumia teknolojia katika shughuli za kiuchumi,tutakuwa na Tanzania
inayotegemea uchumi wa kidijitali “digital economy”.Kufika huko inawezekana
kabisa,lakini tunapaswa kutambua hatutafika huko ndani ya siku moja,mwezi
mmoja,mwaka mmoja,bali itatuchukua miaka mingi sana kuwa taifa linalotegemea na
kuendeshwa na digital economy.
kuwa sehemu ya
mabadiliko unayotaka kuyaona Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania
Makala
hii imeandikwa
na Baraka Daniel Kiranga(23)
0762362413
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation.
0 comments:
Post a Comment