Dar es Salaam.Rais Jakaya Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa jana usiku na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema kuwa Kamishna Mangu anachukua
nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini aliyestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza kesho, Januari Mosi,
2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai
(Director of Criminal Intelligence) katika jeshi hilo la Polisi. Pia
taarifa hiyo ilisema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman
Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika
muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa
Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic
Investigations). Taarifa hizi zilitufikia wakati tukienda mtamboni.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation.
0 comments:
Post a Comment