"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono.
Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.
Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi
kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na
Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.
Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.
Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za
kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na
fedha za chama kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba.
Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote.
Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga
ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005
kufuatia deni lake NSSF.
Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.
They must know I am not a push over. Chacha died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."
HABARI KAMILI
Monday, January 6, 2014
Saturday, January 4, 2014
KIJANA ACHEZEA MKONG'OTO BAADA YA KUJIFANYA KIJOGOO KWA MKE WA MTU
KIJANA ACHEZEA MKONG'OTO BAADA YA KUJIFANYA KIJOGOO KWA MKE WA MTU
HAPA AKIOMBA MSAMAHA BAADA YA KUWEKEWA MTEGO NA KULA KICHAPO CHA KUFUNGIA MWAKA
NIKITOKA HAPA SITARUDIA TENA, NDIVYO ANAVYOONEKANA KUSEMA KIJANA HUYU MKAAZI WA KITUNDA.
HAPA AKIOMBA MSAMAHA BAADA YA KUWEKEWA MTEGO NA KULA KICHAPO CHA KUFUNGIA MWAKA
NIKITOKA HAPA SITARUDIA TENA, NDIVYO ANAVYOONEKANA KUSEMA KIJANA HUYU MKAAZI WA KITUNDA.
MFAHAMU JAJI AUGUSTINO RAMADHANI, TOKA BRIGEDIA JENERALI, JAJI MKUU HADI UCHUNGAJI.
Zanzibar.Baba wa Taifa alipendelea sana kuitwa
Mwalimu, kazi aliyoanza kufanya kabla ya kuwa Rais wa kwanza na hadi
anastaafu urais jina la Mwalimu hakuliacha hadi mauti yalipomkuta.
Hii inakuwa ni vigumu kwa mtu aliyetumikia nafasi
nyingi kwa nyakati tofauti na kwa mafanikio mazuri, nasema mazuri kwa
sababu Jaji Augustino Ramadhani aliyestafu Ujaji Mkuu alipaswa pia
kuitwa Brigedia Jenerali kwa kuwa pia alilitumikia Jeshi hadi kufikia
ngazi hiyo ya Brigedia Jenerali kabla ya kuitwa katika sekta ya sheria
na kutumikia Mahakama hadi kufikia ngazi ya juu kabisa ambayo pia wengi
hupenda kuandikwa kwa vyeo walivyowahi kutumikia na kwa sasa amepewa
kazi ya ukasisi.
Mbali na kustaafu ujaji, wiki iliyopita alipewa
kazi ya ukasisi, alitawazwa rasmi kuwa Mchungaji wa Dayosisi ya Kanisa
la Anglikana lililopo Mkunazini Zanzibar na hivyo kustahili kuitwa cheo
cha Mchungaji Augustino Ramadhani.
Mchungaji Augustino aliiambia Mwananchi kuwa
alizaliwa Visiwani Zanzibar, Mtaa wa Kisima Majongoo kwenye familia ya
watoto wanne wa Mwalimu Mathew Douglas Ramadhani na Bridget Anna
Constance Masoud akiwa ni mtoto wa pili katika familia hiyo, aliishi kwa
miaka mitatu Visiwani huko na kisha alikuja Tanzania Bara (Tanganyika)
akiwa na umri wa kuanza masomo hadi alipohitimu masomo ya sekondari
katika Shule ya Wavulana Tabora na wakati akiwa sekondari ndipo
alilpojifunza kupiga kinanda akirithi kipaji cha babu yake Augustino
Ramadhani.
Jaji Ramadhani alihitimu elimu ya sekondari mwaka
1965 na kujiunga na elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
katika fani ya sheria hadi mwaka 1970 alipojiunga katika Jeshi la
kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria, baadaye aliajiriwa katika Jeshi la
Ulinzi la Wananchi (JWTZ) alikofanya kazi za sheria.
Mafanikio zaidi
Alifafanua kuwa aliitwa na aliyekuwa Rais wa pili
wa visiwa hivyo, Alhaji Aboud Jumbe mwaka 1978 na kumteua kuwa Naibu
Jaji Mkuu kabla ya kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na mwaka huo huo aliitwa
tena jeshini kwa ajili ya kushiriki vita ya Kagera, alipelekwa Uganda na
kukaa kwa zaidi ya miezi kumi.
Baada ya vita kumalizika alirudi Tanzania
kuendelea na kazi katika sekta ya Sheria na mwaka 1980 aliapishwa kuwa
Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Anasema, mfumo wa Mahakama Visiwani haukuwa wa
kisheria na alifanikiwa kuubadilisha na kuweka mfumo wenye ngazi za
Kimahakama kutoka Wilaya, Mkoa hadi Mahakama Kuu. Anabainisha kuwa hii
ilitokana na kutokuwepo na watu waliosomea sheria ili kuajiriwa katika
sekta ya sheria.
“Nilifanikiwa kuondoa mfumo wa mabaraza (Peoples
Court) na kuweka mfumo wa mahakama uliofuata ngazi za kimahakama na
mahakama ya Rufaa haikuwepo kabisa”, anasema.
Pia aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa
mwaka 1989, mwaka 1990 alihamia jijini Dar es Salaam na Mwaka 1993 hadi
2003 aliteuliwa pia kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania
Bara na mnamo mwaka 2002-2007 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar na katika kipindi hicho hicho alikuwa mmoja wa Majaji
sita wa Mahakama ya Afrika Mashariki, pia alikuwa ni mmojawapo wa Majaji
11 waliochaguliwa na Marais wa Afrika kwa ajili ya kuitumikia Mahakama
ya Afrika ya Haki za Binadamu na ndipo mwaka 2006 alipoteuliwa na Rais
Jakaya Kikwete kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Baada ya kustaafu kazi ya Ujaji Mkuu mwaka 2010,
Jaji Augustino Ramadhani alikataa kuendelea na kipindi kingine baada ya
kufanikiwa kufafanua kifungu kinachokataza Jaji kuendelea na kazi ya
Ujaji baada ya umri wake wa kustaafu na kuendelea kwa mkataba wa
ajira, ila anaruhusiwa kuongeza kipindi kimoja tu hata kama bado anazo
nguvu za kutumikia Taifa.
Mara baada ya kusimikwa kuwa Mchungaji anasema, hakuna tofauti
kati ya kazi ya Mahakama na kazi ya Uchungaji kwani zote ni kazi za
kufanya maamuzi ya watu wanaodai wapatiwe haki na kubainisha kazi za
mahakama ukiamua umeamua ila za kanisa zinataka makubaliano na
maridhiano japo zote ni kazi za Mungu.
“Kazi hii ya uchungaji mimi sikuifikiria hata siku
moja kwamba nitaifanya ingawa nilisomea nchini Uingereza na kutunukiwa
stashahada. Pia nilikuwa nikishiriki katika shughuli za madhabahuni
hasa wakati wa kuwasimika maaskofu kwa kuwa nilikuwa mwanasheria wa
kanisa hili hadi nilipoteuliwa kuwa Jaji Mkuu ndipo nilipoamua kuacha
wadhifa huo ili kuepuka migongano,”anasema Jaji Ramadhani.
Atafutwa
“Askofu alinifuata mara kwa mara ingawa nilikuwa
nikimkatalia lakini mwisho nilikubali kwa kuona kuwa ni sauti ya Mungu
iliyokuwa ikiniita kupitia kwake na ndio leo hii baada ya kutumikia
ushemazi kwa zaidi ya miezi sita nimesimikwa rasmi kuwa mhudumu wa
madhabahuni.”
Kwa upande mwingine Jaji anasema, lengo lake
lilikuwa baada ya kustaafu akafundishe na lengo hilo limetimia kwani pia
kwa sasa ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Iringa anapofundisha
sheria.
Pia itakumbukwa kuwa wiki hii amekamilisha kazi ya
kuunda rasimu mpya ya katiba alipoteuliwa mwaka jana kuwa Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.
Hali ya Zanzibar
Akizungumzia hali ya vugu vugu la hali ya visiwani
humu kuhusu kushambuliwa kwa viongozi wa dini na kuharibiwa kwa nyumba
za ibada anasema tangu miaka ya nyuma akiwa mdogo anakumbuka jinsi
walivyokuwa wakishirikiana vizuri na majirani zao kuadhimimisha sikukuu
za kidini bila kujali tofauti ya za dini.
“ Nakumbuka wazazi wangu walikuwa wanamwita
Mwislamu kuja kuchinja kuku ili wasikwazike wanapokaribishwa kujumuika
katika chakula, kwa kuwa walijua kuwa nyama wanayokula imechinjwa kwa
taratibu za dini yao na haitamkwaza na wao pia walikuwa wakitualika
kwenye sikuku zao na tulikuwa tukifurahia pamoja.”
Mwananchi pia ilishuhudia amani iliyokuwepo wakati
misa ya kumwapisha Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani ilipokuwa
ikifanyika na hakuwa na uvunjivu wa aina yoyote ya amani licha kuwepo na
ulinzi wa kawaida na hakukuwa na Polisi kama ilivyokuwa wakati wa
mkesha wa Siku Kuu ya Krismasi.
Wageni walikuwa wengi na kanisa lilijaa watu waliokuja kushuhudia tukio hilo la kusimikwa kwake.
Chadema ngoma nzito,wafuasi watwangana makonde mahakamani
Dar es Salaam. Vurugu za aina yake zimezuka
katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, baada ya watu wanaodhaniwa
kuwa wanachama wa Chadema kumzomea aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama
hicho, Zitto Kabwe.
Vurugu hizo zilihusisha wafuasi wa chama hicho
wanaomuunga mkono Zitto na wale wanaompinga, ambao walikuwa wamebeba
mabango ya kumsifia na wengine wakiwa wamebeba ya kumkashifu.
Katika vurugu hizo, baadhi ya wanachama hao
waliamua kufanya doria isiyo rasmi ndani ya mahakama hiyo ya kuwasaka
watu waliodai kuwa ni mamluki, huku wakimkamata askari kanzu, kabla ya
kumpiga ngumi na kumchania shati mtu mmoja wakidai kuwa alikuwa
akiwarekodi kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana asubuhi
ambapo kundi la wanachama hao, huku baadhi wakiwa wamevaa nguo za kaki
zinazotumiwa na chama hicho kufika katika mahakama hiyo kwa lengo la
kusikiliza kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na Zitto.
Mara baada ya kuwasili kwa Mbunge huyo wa Kigoma
Kaskazini, huku akiwa ameongozana watu kadhaa wakiwamo wanasheria wake
na mabaunsa, wanachama hao walianza kumzomea huku baadhi wakimwita
fisadi.
Hali hiyo iliibua zogo katika eneo la mahakama
hiyo, hali iliyowalazimu maofisa kadhaa wa polisi kuingilia kati kwa
kuamua kumchukua Zitto na kumhifadhi kwenye chumba maalumu na kumtoa saa
6 mchana kesi yake ilipoanza kusikilizwa. Baadhi ya mabango ya
kumkashifu yalisomeka; Zitto tulimpenda, CCM imempenda zaidi, Zitto
rudisha fedha za CCM.
Yale yaliyomsifia yalisomeka; Zitto kama Mandela
na Zitto ni Mkombozi.Baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, saa
12 jioni wanachama hao walianza kurushiana ngumi, hasa baada ya
kuibuliwa kwa mabango yaliyosomeka ‘Zitto kwanza Chadema baadaye’.
Awali hali hiyo ilimfanya Zitto kutaharuki, huku mabaunsa wake wakijihami na kuanza kumlinda.
Baada ya Zitto kuhifadhiwa baadhi ya wanachama hao
ambao waliingia kwa kuandikishwa majina yao getini, walianza kuwasaka
watu waliowahisi kuwa mamluki, ambapo walimnasa askari kanzu na kuanza
kumzonga wakimuhoji anapeleleza nini katika eneo hilo.
“Hapa tunataka kujua wewe ni nani na unataka nini
hapa, maana hatukuelewi kabisa kwa nini unakuja kusikiliza mazungumzo
yetu, jitambulishe,” alisisika mmoja wa wanachama hao akimhoji askari
huyo huku akiwa amemkandamiza ukutani,
“Tunajua wewe ni askari kwa nini hujavaa sare leo? Kisha unajichanganya kwenye kundi letu.”
Kesi hiyo ilimalizika saa 12 jioni ambapo Zitto
alitolewa chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa kupitia mlango wa nyuma wa
mahakama hiyo na kuwaacha wafuasi hao wakionyeshana ubabe kwa mabango
na kauli za kejeli.
Ndani ya mahakama
Kabla ya kuanza kwa kesi hiyo, Mwanasheria Mkuu wa
Chadema, Tundu Lissu alimwomba Jaji John Utamwa kuendesha kesi hiyo kwa
lugha ya Kiswahili kwa kuwa inagusa sehemu ya masilahi ya umma, jambo
ambalo liliibua shangwe kwa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika
katika mahakama hiyo.
Hata hivyo baada ya kesi kuanza kuendeshwa kwa
lugha ya Kiswahili, Jaji Utamwa alilazimika kuikatiza, na kuwakemea
wanachama wa Chadema baada ya sauti za kuguna kusikika wakati wakili wa
Zitto, Albert Msando alipokuwa akiwasilisha hoja kuhusu msingi wa kesi
hiyo.
“ Nataka kuwakumbusha hapa mahakamani ni tofauti
na sehemu nyingine sauti zinazosikika sizitaki, anayeona kwamba
yanayozungumzwa hakubaliani nayo kama hawezi kunyamaza atoke nje
vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Jaji Utamwa.
Kundi la Wanachadema hao huku wengine wakiwa
wamevalia sare zao waliwasili mahakamani hapo ili kusikiliza kesi ya
pingamizi iliyofunguliwa na Kabwe akiiomba Mahakama iwazuie Bodi ya
Wadhamini wa Chadema, Katibu Mkuu pamoja na Kamati Kuu ya Chadema jana
kumjadili, kumchukulia hatua, uamuzi wowote wala kuhusu uanachama wake.
Msingi wa kesi
Juzi Zitto aliomba Mahakama hiyo kuzuia Kikao cha
Kamati Kuu ya Chadema kumjadili hadi rufaa yake aliyoikata kwenye
Baraza Kuu la Chadema itakaposikilizwa na kuamuliwa na wazuiwe
kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya ubunge wa Kigoma
Kaskazini .
Pia aliiomba Mahakama hiyo Kuu kumwamuru Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa ampatie nakala ya mashtaka na maelezo
ya uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu Novemba 22, 2013 na kusababisha
avuliwe nyadhifa zake ili aweze kupeleka rufaa yake Baraza Kuu la
Chadema kupinga uamuzi huo.
CCM yamtolea uvivu Lowassa urais 2015
Dar es Salaam. Unaweza kusema sasa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kimeamua kumfungia kazi Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa baada ya jana Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Phillip Mangula
kusema kuwa wanachama wake walioanza mbio za kuwania urais mwaka 2015
watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Mangula alisema kama wanachama hao wasipochukuliwa hatua watakifanya chama hicho kupoteza mvuto katika medani ya kisiasa nchini;
“Wapo watu wanataka waichanechane CCM kwa sababu
ya uroho wao wa madaraka, uroho wa udiwani, ubunge na hata urais. Kuna
makundi ndani ya chama kazi yake ni kuwabomoa wenzao, kamwe hatuwezi
kuyafumbia macho.”
Akifafanua hilo Mangula alisema: “Tutawaita wote
walioonyesha nia ya kuutaka urais 2015 na kuwahoji kwanini wanafanya
hivyo wakati muda bado haujafika. Tumeshawachunguza katika mikutano
wanayoifanya, tumebaini kuwa wanatoa misaada na kusafirisha watu,
tunajua dhamira yao ni nini.”
Mangula ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja
tangu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kusema
mwanachama yeyote wa CCM anayetangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda
mwafaka kutangazwa atapoteza sifa za kugombea.
Nape alitoa kauli hiyo baada ya Lowassa siku mbili
zilizopita, kutangaza nia ‘kimtindo’ akisema anaanza rasmi safari
aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za
Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa
wagombea wa nafasi ya urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015,
alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya,
katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa
Monduli.
Mangula aliwashukia vigogo wa chama hicho
wanaoutaka urais jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Kamati ya
Siasa tawi la Ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, wakati akitoa salamu
za mwaka mpya kwa wanachama wote wa CCM nchini.
Ataja kanuni za uongozi
Katika mkutano huo Mangula alisaidiwa kusoma
kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho, kutolea ufafanuzi mambo
mbalimbali na Katibu Tume ya Udhibiti wa Nidhamu ya Viongozi wa CCM na
wanachama taifa, Masoud Mbengula.
Moja ya kanuni hizo inasema “Ni mwiko kwa kiongozi
wa CCM kutumia dini yake au kabila au rangi au jinsia au eneo
analotoka, kama sifa ya kushawishi wapiga kura wamchague ama yeye
mwenyewe ama mgombea anayemuunga mkono.”
Mangula alisema kwa mujibu wa kanuni za chama
hicho, mwanachama anayefanya mambo kinyume na kanuni huitwa msaliti na
hafai kuendelea kufumbiwa macho kwani anaweza kukiangamiza chama wakati
wowote.
“Tutawachukulia hatua kali wale wote ambao wameanza kuonyesha
dalili kama hizo za kutoa michango, misaada, zawadi. Lengo la mwanachama
huyo ni kutaka kuungwa mkono, wanaotaka madaraka wasubiri muda ufike
ndiyo wafanye hivyo.”
Aliongeza “Hivi haya mapenzi ya kusaidia yameanza
lini, fedha hizo zinatoka wapi, hawa wanaosadiwa wanatakiwa kutambua
kuwa yote hayo ni kampeni kwa kuwekeza, hatuwezi kuwa na viongozi wa
nchi wa namna hii wa uchu wa madaraka, CCM haitawafumbia macho lazima
kanuni na miongozo ifuatwe.”
“Kuna watu wameanza kudhani kuwa muda wa kampeni
umeanza, muda wa kampeni haujafika na hakuna majina yaliyotangazwa ya
kugombea udiwani, ubunge hata urais,” alisema Mangula na kuongeza;
“Kuna makundi yanaifanya nchi ya Somalia
isitawalike. Makundi ya aina hiyo naona yapo hata CCM; watu wanaibua
vita ya maneno ndani ya chama, wanataka wakichanechane chama kwa sababu
ya uroho wa madaraka tu.”
Bila kuyataja makundi hayo Mangula alisema:
“Utaongozaje nchi ambayo imegawanyika katika makundi? Watu wameanza
kuvuruga chama chetu, kila mtu ana kundi lake na wakati mwingine
wanayatumia makundi kuwabomoa wenzao, hili jambo hatuwezi kulifumbia
macho hata kidogo.”
Mbali na Lowassa, wengine wanaotajwa kuwania
nafasi hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi na Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba.
Makamba hivi karibuni amekuwa akitoa misaada kwa
vikundi vya waendesha bodaboda katika mikoa mbalimbali, hali ambayo
inatafsiriwa kuwa ni kujiimarisha kisiasa.
Hata hivyo, mwaka jana Rais Jakaya Kikwete ambaye
pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa alinukuliwa akisema kuwa sio vibaya kwa
wanachama wa chama hicho kuonyesha nia ya kuwania nafasi za uongozi
ndani ya chama, lakini siyo kufanya kampeni.
Mei 26 mwaka jana, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana akiwa mkoani Iringa, alisisitiza kwamba chama kitamwadhibu bila
huruma mwanachama yeyote anayejipitisha katika maeneo mbalimbali na
kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
Akifunga mafunzo ya makatibu na wenyeviti wa
wilaya na mikoa mjini Dodoma mwaka jana, Rais Kikwete alisema kuwa
inasikitisha kuona kuwa wapo baadhi ya watu ambao wameanza kujipitisha
kwa viongozi wa chama na kuwapatia hela kwa ajili ya kuwapigia debe ili
wawachague katika nafasi mbalimbali za urais ama bunge.
Alisema kuwa kimsingi kwa sasa wapo watu ambao
wameishaanza kuzunguka na kujinadi kutafuta nafasi mbalimbali za
kugombea, huku wakipenyeza rushwa jambo ambalo linaendelea kukishushia
hadhi chama hicho.
Uchaguzi Serikali za Mitaa
Mangula akizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika
mwaka huu alisema, viongozi wote wanatakiwa kufuata taratibu na kanuni
na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
“Vitendo vya rushwa ndio vilitufanya katika
chaguzi zilizopita kufanya vibaya, watu walinunuliwa kadi, sasa viongozi
wa matawi wawe makini tusirudi tulikotoka na tukibaini mtu hafuati
kanuni tutamwajibisha,” alisema Mangula.
Subscribe to:
Posts (Atom)